Isaiah 32:14-19


14 aNgome itaachwa,
mji wenye kelele nyingi utahamwa,
ngome ndani ya mji na mnara wa ulinzi vitakuwa ukiwa milele,
mahali pazuri pa punda na malisho ya makundi ya kondoo,

15 bmpaka Roho amwagwe juu yetu kutoka juu,
nalo jangwa kuwa shamba lenye rutuba,
na shamba lenye rutuba kuwa kama msitu.

16 cHaki itakaa katika jangwa,
na uadilifu utakaa katika shamba lenye rutuba.

17 dMatunda ya haki yatakuwa amani,
matokeo ya haki yatakuwa utulivu
na matumaini milele.

18 eWatu wangu wataishi katika makao ya mahali pa amani,
katika nyumba zilizo salama,
katika mahali pa kupumzika pasipo na usumbufu.

19 fHata kama mvua ya mawe iangushe msitu
na mji ubomolewe kabisa,
Copyright information for SwhKC